
Maneno ambayo yame shamiri sana ao yame tumiwa nahawa Kandideti wa2 uraisi: Moïse Katumbi na Félix Tshisekedi.
Hawa wa2 nimiongoni ya wale 24 wenye wana gombea kiti cha Uraisi nchini DRC.
Na hawa ndio wako nawafuasi wengi nchini.
Moïse Katumbi, ni nani ?
Kiufupi anajulikana kwa majina ya Moïse Katumbi Chapwe.
Kisiasa Aliwai kuwa Gavana wa jimbo la Katanga na Anasifiwa sana kwenye uongozi wake kama Gavana enzi hizo alitekeleza mambo mengi yamaendeleo jimbo hilo la Katanga, pia nchi nzima anazo Sifa Tele.
Kijamii ni mutu anaye juwa ku nyenyekea nakushirikiana nawatu wote.
Anajulikana pia kupitia Sport ku kuza Talanta za vijana na yeye ndie kiongozi wa TP MAZEMBE.
Katumbi, aliongea mengi lakini nitasema machache but yenye ame penda kuzungumuzia mara kwa mara.
Mukinichagua kama Raisi wa DRC :
Kitu chakwanza “Nitarudisha Usalama nchini kote. Ni tawezesha askari wa nchi kwanjia zote ili nawo wapate nguvu na motisha yakulinda Usalama wa wananchi na kulinda mipaka ya DRC.”
“Nikuwalipa wanajeshi vizuri nakuwapa vifaa byakisasa. Nitapunguza mishahara ya wabunge ili ongezee wanajeshi pamoja na Polisi.”
“Nitaweka kipaombele maendeleo ya nchi kwa Sekta zote kamavile:
Miundo msingi barabara,Shule na Hospitali.”
“Nitarudisha Uusiano muzuri kati ya DRC na nchi jirani ambao umepotea kwamuda murefu.”
Félix Tshisekedi ni nani ?
Yeye ndie Raisi wa DRC ambaye anakamilisha muhula wa kwanza.
Kwenye mhula huu ambao anahitimisha hakufanikiwa kutimiza ahadi alizo pea wananchi wake,hivo basi akajipotezea uaminifu kwawatu wengi nchini DRC.
Alifahamika kuwa Raisi mwenye safari nyingi duniani.
Anapenda Sana kuhuzuria kongamano Sherehe Sport pia kwenye Matanga yawatu maarufi na Harusi Pia.
Félix Tshisekedi, aliongea mengiii but yale alitumia sana nihaya:
“Mukinichagua nitarudi usalama nchini kote. Nita undoa wageni ambao wako kwanye ngazi za Serekali kama vile kwenye Jeshi na Polisi,tumeanza kuwaondoa mumojamumoja (Kuwauwa),nawengine wame anza kujiondoa wenyewe.”
” Waasi kama vile wa Maï Maï na Wazalendo nitawazawadi kwakuwaweka kwenye Serekali ili tumufukuze mugeni.”
” Nikichagulia Nitaomba bunge Liniruhusu ili nivamie Rwanda.Kagame kama anacheza nawatu Wengine Asicheze na Tshilombo,asema Félix Tshisekedi. Musiwaskize wale kandideti wa Kagame.”
Haya ndio maneno ya viongozi hawa wa2.
Je Kwaupande wako ninani ako na sera nzuri.
Tunaomba amani iitawale nchi ya DRC tukisubiri uchaguzi hapo kesho.
By Wilson