Raisi wa M23, muheshimiwa Bertrand Bisimwa, analaani kitendo kilicho fanywa na muungano wa wanajeshi wa DRC chakushambulia ngome za M23 na kuvunja makubaliano yakusimamisha vita kwasiku 14 kama vile wali amurishwa na Marekani.
Wiki iliopita tarehe 13/12/2023 ndio wali shurutishwa na serekali ya Marekani kusimamisha mashambulizi pande zote husika,baada yakumaliza siku zingine 3 bila mashambulizi.
Kama vile kiongozi wa M23 Bertrand Bisimwa ametangaza leo tarehe 22/12/2023, amesema niki mnuku:”Tangu jana tarehe 21/12/2023 muungano wa jeshi la DRC wame vamia ngome zetu ARC/M23,mkowa wa Masisi/Kivu Kaskazini.”
“Kulingana na muonekano wa jeshi la DRC nikwamba wame amua kuendeleza mashambulizi.”
Aliendelea kusema “Muungano wa jeshi hili kuanzisha mashambulizi ni ishara tosha yakuvuruga uchaguzi ambao ukokaribu kukamilika.”
Bertrand Bisimwa amemaliza Alakisema : “ARC/M23 iko imara na itaendelea kujikinga zidi yamashambulizi na kulinda usalama wa wakaaji (Raia) pia na kulinda mali yao.”
Habari zakuaminika ambazo Minembwe Capital News, tunazo nikwamba M23 ime faulu kuteka vijiji ambavyo vilikuwa mikononi mwa FARDC pamoja na washirika wake.
Vijiji hivyo nipamoja na:
Kinduzi na
Gatama, Tarafa la Masisi mkoa wa Kivu Kaskazini.
Habari zaidi zinasema kuwa M23 ime zibiti vijiji vingine mbili Kutokana namapigano yahapo jana,karibu na “Rubaya pa Bashali”.nivijiji amabavyo vime Shuhudia makabiliano makali hapo jana 21/12/2023.
Bruce Bahanda.